Featured Books
Featured books only - 7 books available
SULUHU YA NCHI/DUNIA
Kitabu hiki kinatoa mtazamo kuhusu namna ya kuleta suluhisho la kudumu kwa migogoro, vita, uonevu na mateso katika jamii. Mwandishi anajadili ubinafsi kama chanzo kikuu cha matatizo ya dunia na kupendekeza njia rafiki inayolenga kurejesha utu wa mwanadamu, haki, usawa na amani bila kutegemea mabavu.…
"DINI" NI KIKWAZO KIKUU CHA UKOMBOZI HALISI WA MWANADAMU
Kitabu kinachochambua kwa mtazamo wa mwandishi nafasi ya dini katika jamii, changamoto za viongozi na waumini wa dini, haki za binadamu, uwajibikaji na ukombozi wa kweli wa mwanadamu. Mwandishi anatoa hoja na mifano kutoka katika Biblia ili kuchochea mjadala kuhusu tofauti kati ya imani inayotamkwa na matendo yanayotekelezwa katika maisha ya kila siku.…
Vyama vya Kufa na Kuzikana na Vikundi-vikundi ni Ushetani
Kitabu kinachochambua vyama vya kufa na kuzikana, vikundi vya kusaidiana na kukopeshana kwa mtazamo wa Kikristo, kikisisitiza upendo wa kweli, kusaidiana bila kutarajia malipo na kutenda mema kwa Mungu na wanadamu.…
Kitabu cha Mcha Mungu Kutoka Gerezani
Ushuhuda na wito wa mchungaji aliyefungwa kwa siku 137, akieleza hali ya wafungwa na mahabusu magerezani na kupendekeza mageuzi ya haki, utu na urekebishaji wa kweli.…
Kutubu Kwa Mtu au kwa Mungu kutakako sababisha upone magonjwa
Kitabu hiki ni upatanisho /mpatanishi wa kweli. Watakaopatana kwa kuongozwa na kitabu hiki anaweza wasikosane tena mpaka kufa. Si kwamba mmoja hatamkosea mwingine kabisa, hasha! Bali hawa wawili watajaa mema kila mmoja kwa mwenzake kiasi cha ubaya huo kutoonekana na hata ukionekana basi wingi wa mema wanayotendeana “utameza” kosa au kulifanya dogo sana.…
Madhara ya kutoa Sadaka Ukiwa na Dhambi
Natambua kuwa kitabu hiki kitatia mchanga vitumbua vingi vya wahubiri wengi ambao walijua kuwa hawawezi kufikiwa mahali walipojificha na kuficha mbinu nyingi “chafu” za kujipatia mali na utajiri mwingi kupitia neno SADAKA, FUNGU LA KUMI, MCHANGO na aina mbalimbali za matoleo .…
Bila Maombi Mengi Utaangaika sana Duniani
Kitabu hiki ni majibu ya maswali mengi waliyonayo watu kuhusu maombi. Na ndio maana katika maeneo mengi kimeandikwa kwa mfumo wa maswali na majibu. Ni kitabu tunachoamini kuwa kila ukurasa au aya au kichwa cha somo utakachokisoma, kitakufanya uanze kupenda kuomba sana.…