Bila Maombi Mengi Utaangaika sana Duniani

by Mch Mbarikiwa Mwakipesile

TZS 5,000 132 pages English PDF

Kitabu hiki ni majibu ya maswali mengi waliyonayo watu kuhusu maombi. Na ndio maana katika maeneo mengi kimeandikwa kwa mfumo wa maswali na majibu. Ni kitabu tunachoamini kuwa kila ukurasa au aya au kichwa cha somo utakachokisoma, kitakufanya uanze kupenda kuomba sana.

  • Instant download after payment
  • Secure PalmPesa mobile money payment
  • Read on any device - phone, tablet or laptop

About This Book

Namuomba Mungu kwamba kila aliyeokoka au aliyeingia kanisani kwa kusudi la kumtafuta Mungu aweze kusoma kitabu hiki. Lakini Pia namuomba Mungu kitabu hiki kisomwe na wahubiri wote wanaohubiri kwa ajili ya maslahi ya Mungu na hata wakitumie kuwaimarishia watu wao. Kwani watu wao/wa Mungu wakifahamu jinsi ya kuwa na maombi mengi, watapata ufunguo wa kila kufuli, komeo, kitasa au pingu iliyofunga maisha yao kwa namna yoyote. Lakini pia ni maombi yangu kuliombea kanisa kote duniani ili watambue kuwa; kanisa lolote au mtu yeyote aliye na uwezo wa kutoa mapepo au kupona magonjwa kokote kunakotokana na maombezi, kama tu kanisa hilo au mtu huyo hana maombi mengi yaliyo zaidi ya haya yaliyopendekezwa katika kitabu hiki; Basi KINACHOFANYIKA HAPO NI MAZINGAOMBWE NA VIINI MACHO. Na ili uthibitishe kuwa ni viini macho, basi watu wote wanaoombewa hapo hurudiwa na mateso yale yale na hata zaidi ya yale na huwa WANAKUWA NA MAISHA MACHAFU SANA (YA KALE) na huwa hawadumu siku nyingi katika wokovu. Lakini pia namuomba Mungu akujulishe na kukufunulia ukweli uliomo katika maombi mengi ambapo pasipo maombi mengi, mguso wowote unaokuwepo kwenye ibada, au kushangilia kokote kunakokuwepo wakati wa ibada au sherehe au kufaulu masomo, kupata kazi au faida kubwa katika biashara au kilimo, HAKUTAKUWA NA RAHA AU FURAHA ITAKAYODUMU. Ghafla utajikuta kwenye maumivu makali ya moyo, mwili au ufahamu bila kujua chanzo chake na huku ukiwa huna nguvu ya kuirudisha hali ya furaha uliyokuwa nayo hata kama vitu hivyo vitakuwepo au kuongezeka. Bwana na akupe kuyaelewa maneno yaliyoandikwa katika kitabu hiki na MUNGU NA AWE JUU YA MANENO HAYA, KATIKA JINA LA YESU KRISTO, AMENI.

What You Will Learn

  • Utajifunza Maana ya Maombi Mengi
  • Utajifunza namna ya kuanza kuomba
  • Utajifunza jinsi ya kupokea majibu baada ya kuomba
  • Utajifunza maana ya kuomba vibaya

Book Information

AuthorMch Mbarikiwa Mwakipesile
Pages132
FormatPDF (digital download)
LanguageEnglish
CategoryGeneral
Published03 Oct 2026
PriceTZS 5,000

Sample Preview

Read a free sample of this book. The full book is available after purchase.

You are viewing the free sample. Buy the full book to unlock all pages.

You May Also Like

SULUHU YA NCHI/DUNIA cover Ukombozi

SULUHU YA NCHI/DUNIA

Mch Mbarikiwa Mwakipesile

Kitabu hiki kinatoa mtazamo kuhusu namna ya kuleta suluhisho la kudumu kwa migogoro, vita, uonevu na mateso katika jamii. Mwandishi anajadili ubinafsi kama chanzo kikuu cha matatizo ya dunia na kupendekeza njia rafiki inayolenga kurejesha utu wa mwanadamu, haki, usawa na amani bila kutegemea mabavu.…

"DINI" NI KIKWAZO KIKUU CHA UKOMBOZI HALISI WA MWANADAMU cover Ukombozi

"DINI" NI KIKWAZO KIKUU CHA UKOMBOZI HALISI WA MWANADAMU

Mch Mbarikiwa Mwakipesile

Kitabu kinachochambua kwa mtazamo wa mwandishi nafasi ya dini katika jamii, changamoto za viongozi na waumini wa dini, haki za binadamu, uwajibikaji na ukombozi wa kweli wa mwanadamu. Mwandishi anatoa hoja na mifano kutoka katika Biblia ili kuchochea mjadala kuhusu tofauti kati ya imani inayotamkwa na matendo yanayotekelezwa katika maisha ya kila siku.…

Vyama vya Kufa na Kuzikana na Vikundi-vikundi ni Ushetani cover Uponyaji

Vyama vya Kufa na Kuzikana na Vikundi-vikundi ni Ushetani

Mch Mbarikiwa Mwakipesile

Kitabu kinachochambua vyama vya kufa na kuzikana, vikundi vya kusaidiana na kukopeshana kwa mtazamo wa Kikristo, kikisisitiza upendo wa kweli, kusaidiana bila kutarajia malipo na kutenda mema kwa Mungu na wanadamu.…