Madhara ya kutoa Sadaka Ukiwa na Dhambi
Natambua kuwa kitabu hiki kitatia mchanga vitumbua vingi vya wahubiri wengi ambao walijua kuwa hawawezi kufikiwa mahali walipojificha na kuficha mbinu nyingi “chafu” za kujipatia mali na utajiri mwingi kupitia neno SADAKA, FUNGU LA KUMI, MCHANGO na aina mbalimbali za matoleo .
- Instant download after payment
- Secure PalmPesa mobile money payment
- Read on any device - phone, tablet or laptop
About This Book
Pia katika kitabu hiki nitasema “bila woga” jinsi yalivyopaswa kuwa matumizi ya sadaka/matoleo yanayotolewa makanisani ili watoaji wawe na moyo wa kutoa tena na tena na hatimae mbingu ziyafurahie matoleo hayo. Ninafahamu kuwa asilimia kubwa ya wahubiri wa sasa hawatapenda kukielewa kitabu hiki. Yaani watakaposoma maelezo ya mwanzo tu wataingiza mpango wa kujaribu kwa kila njia wawezayo kuwafanya watu wasikipate kitabu hiki na hata wakikipata wasikisome na wakikisoma wasikielewe na wakikilewa wasichukue hatua ya kuyaishi hayo. LAKINI KWA MAMLAKA YA JINA LA YESU NAAMURU ROHO HIYO (iwe itakaa kwa mtu aitwae askofu, mchungaji, nabii, mtume, mwalimu, mwinjilisti, mwimbaji binafsi, bendi, kwaya, au mtu wa aina yeyote kwa sababu zozote), IKADHOOFIKE KWA JINA LA YESU. NA KITABU HIKI KIKAPATE NGUVU YA KUWAFIKIA AINA ZOTE ZA WATU NA KUELEWEKA KWA JINSI ALIVYOKUSUDIA MUNGU, AMENI.
Book Information
| Author | Mch Mbarikiwa Mwakipesile |
|---|---|
| Pages | 138 |
| Format | PDF (digital download) |
| Language | Kiswahili |
| Category | Ukuaji wa kiroho |
| Published | 23 Oct 2026 |
| Price | TZS 5,000 |
You May Also Like
Nyimbo za Imani
Mkusanyiko wa nyimbo 173 za dua, imani na tumaini, ulioandikwa na kuimbwa wakati wa kifungo cha siku 140 cha Mch. Mbarikiwa, wimbo mmoja kwa kila siku.…