Kutubu Kwa Mtu au kwa Mungu kutakako sababisha upone magonjwa - book cover
Uponyaji

Kutubu Kwa Mtu au kwa Mungu kutakako sababisha upone magonjwa

by Mch Mbarikiwa Mwakipesile

TZS 5,000 73 pages Kiswahili PDF

Kitabu hiki ni upatanisho /mpatanishi wa kweli. Watakaopatana kwa kuongozwa na kitabu hiki anaweza wasikosane tena mpaka kufa. Si kwamba mmoja hatamkosea mwingine kabisa, hasha! Bali hawa wawili watajaa mema kila mmoja kwa mwenzake kiasi cha ubaya huo kutoonekana na hata ukionekana basi wingi wa mema wanayotendeana “utameza” kosa au kulifanya dogo sana.

  • Instant download after payment
  • Secure PalmPesa mobile money payment
  • Read on any device - phone, tablet or laptop

About This Book

Lakini pamoja na hayo “nikiri” kwamba; kitabu hiki kinaweza kisieleweke kirahisi kwa wengi wao. Ninajua wengi wataanza kuelewa na kuona uzuri wa kitabu hiki wakisoma mada zaidi ya tatu hasa zinazoanzia sura ya tatu au ya nne kwa kuwa mada ya wanza na ya pili inaweza kueleweka zaidi kwa watu walio na ukaribu sana na Mungu. Hivyo ikiwa utataka upate suruhisho la kweli na la kudumu kupitia kitabu hiki ni vema usome mada zaidi ya tatu. Nina uhakika kuwa kitabu hiki ni mwanzo wa sherehe kwenye mioyo na maisha ya wengi sana.

Familia, koo, nchi na Jamii nyingi zimefarakana vibaya kiasi cha “uhasama/uadui” wao kudumu vizazi na vizazi (au kwa mda mrefu) kwa sababu ya KUTUBU KIHOLELA AU KUSAMEHE KUSIKO SAWA SAWA. Eneo la kutubu huwa linafanyika kiwepesi sana kiasi ambacho badala ya kumaliza tatizo huzalisha tatizo zaidi au kuharibu mambo zaidi.

Book Information

AuthorMch Mbarikiwa Mwakipesile
Pages73
FormatPDF (digital download)
LanguageKiswahili
CategoryUponyaji
Published23 Oct 2026
PriceTZS 5,000

You May Also Like

Vyama vya Kufa na Kuzikana na Vikundi-vikundi ni Ushetani cover Uponyaji

Vyama vya Kufa na Kuzikana na Vikundi-vikundi ni Ushetani

Mch Mbarikiwa Mwakipesile

Kitabu kinachochambua vyama vya kufa na kuzikana, vikundi vya kusaidiana na kukopeshana kwa mtazamo wa Kikristo, kikisisitiza upendo wa kweli, kusaidiana bila kutarajia malipo na kutenda mema kwa Mungu na wanadamu.…