Nyimbo za Imani
Mkusanyiko wa nyimbo 173 za dua, imani na tumaini, ulioandikwa na kuimbwa wakati wa kifungo cha siku 140 cha Mch. Mbarikiwa, wimbo mmoja kwa kila siku.
- Instant download after payment
- Secure PalmPesa mobile money payment
- Read on any device - phone, tablet or laptop
About This Book
Kitabu hiki ni mkusanyiko wa nyimbo zilizoandikwa na kuimbwa na Kikosi Kazi cha Injili wakati kiongozi wao, Mch. Mbarikiwa Mwakipesile, alipokuwa gerezani kuanzia tarehe 29/9/2023 hadi 15/2/2024. Kila siku ya kifungo iliandikwa wimbo mmoja, na idadi ya nyimbo ndiyo idadi ya siku alizokaa gerezani.
Zimeitwa “Nyimbo za Imani” kwa sababu ni nyimbo za kumwonyesha Mungu kuwa tunalia na tunaumia, lakini imani yetu haijatetereka. Pia ni dua na maombi kwa Mungu aangalie mateso na vilio vyao. Nyimbo nyingi zimetungwa na mhandisi Onesmo Mwakajili wa tawi la Kyela, akishirikiana na Danny Daniel, Alex Tewele na Andrew Fuime. Mke wa mchungaji, Salome Mwampeta, ndiye aliyeanza kuziimba kwa sauti na video.
Ndani yake kuna nyimbo za kuomba msaada wa Mungu, kumtumaini wakati wa dhiki, kushukuru, kusifu, kuwaonya viongozi, na kuwakumbusha watu kuhusu hukumu ya Mungu. Kitabu kina faharasa ya nyimbo zote kwa mpangilio wa herufi.
Book Information
| Author | Kikosi Kazi Cha Injili |
|---|---|
| Pages | 0 |
| Format | PDF (digital download) |
| Language | Kiswahili |
| Category | Ukuaji wa kiroho |
| Published | 23 Oct 2026 |
| Price | TZS 3,000 |
You May Also Like
Madhara ya kutoa Sadaka Ukiwa na Dhambi
Natambua kuwa kitabu hiki kitatia mchanga vitumbua vingi vya wahubiri wengi ambao walijua kuwa hawawezi kufikiwa mahali walipojificha na kuficha mbinu nyingi “chafu” za kujipatia mali na utajiri mwingi kupitia neno SADAKA, FUNGU LA KUMI, MCHANGO na aina mbalimbali za matoleo .…